WATEJA WA VODACOM SASA SH.1 KWA SEKUNDE MASAA 24


Dares Salaam 17.8.2010 Wateja wa Vodacom Tanzania sasa wataweza kupiga simu kwa masaa 24 kupitia huduma yake ya Habari Ndiyo hii baada ya Vodacom kuboresha huduma za mtandao wake.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba alisema Jijini kwamba uamuzi huo unatokana na ahadi waliyoitoa mapema mwezi Machi mwaka huu kwamba baada ya kufanya maboresho ya mtandao wake Vodacom Tanzania itawawezesha wateja wake kuongea kwa masaa 24 kwa bei ya shilingi moja kwa sekunde.

“Tuliwaahidi wateja wetu wakati wa uzinduzi wa huduma hii kwamba baada ya kukamilisha maboresho ya huduma za mitambo yetu tutawezesha wateja wetu kuongea kwa masaa 24 kupitia huduma yetu hii ya Habari Ndiyo Hii na sasa muda wenyewe ndiyo huu” Alisema .

Vodacom Tanzania ilizindua huduma hiyo mwezi Machi mwaka huu.

Alifafanua kwamba hivi sasa Vodacom Tanzania imeboresha huduma zake za mtandao wake na kwamba wateja wa Vodacom wanapata huduma bora bila kikwazo chochote.

“Tumeboresha huduma zetu, na sasa wateja wetu wanapata huduma bora za mawasiliano na tutaendelea kuboresha kadri siku zinavyokwenda,” Alisema Mkurugenzi huyo.

Kabla ya mabadiliko hayo mteja wa Vodacom alikuwa akipiga simu kwa shilingi moja kwa sekunde kwa masaa 20 kwa siku.

Alisema zaidi ya wateja milioni saba wa Vodacom watanufaika na huduma hii kwa kuongea zaidi kwa bei ile ile siku nzima.

Alisema Vodacom ina lenga kuwawezesha wateja wake kuwasiliana zaidi na bila kikwazo chochote na hivyo kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Post a Comment

Previous Post Next Post