EXTRA BONGO WATAKUWEPO PAMO BEACH RESORT SIKU YA EID EL HAJJ

MRATIBU WA ONYESHO ASHA SAID MWENYE SUTI AKIZUNGUIMZA NA MWANDISHI WA MWANANCHI, VICKY KIMARO.

BENDI ya muziki wa dansi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kujinafasi’ inatarajiwa kutoa buradani kwa wakazi wa Kigamboni na maeneo jirani katika sikukuu ya Idd el Hajj, kupitia onyesho litakalofanyika katika ufukwe wa Pamo uliopo Kigamboni.

Mratibu wa onyesho hilo ambalo ni la kwanza tangu bendi hiyo izundue rasmi albamu yake ya kwanza miezi kadhaa iliyopita, Asha Said alisema kwamba kabla ya bendi hiyo kutumbuiza usiku, mchana kutakuwa na disco toto.
Alisema kupitia disco toto hilo watoto watakaocheza vizuri mtindo wa kiduku watapatiwa zawadi mbalimbali toka kwa waandaaji hivyo kuwaomba wazazi kuwapeleka waoto wao kwa ajili ya kupata burudani mbalimbali.
Asha aliongeza kuwa mbali na Extra Bongo, pia kutakuwa na vikundi vya kanga moja na kiduku ambavyo vitasindikiza onyesho hilo ambapo kiingilio kitakuwa sh.5,000 wakati wa usiku huku mchana watoto watalipa sh.500 na wakubwa watalipa sh.1,000.
Kwa upande mwingine, siku ya Idd pili pia ukumbi huo utapambwa na burudani ya wasanii wa bongo fleva wakiwemo Amin Mwinyimkuuu toka THT, Dk. Leader na Bwana Misosi ambapo kiibgilio kitakuwa sh.3,000.

Post a Comment

Previous Post Next Post