MABINGWA WA LIGI KUU BARA, YANGA
WASHINDI WA PILI SIMBA
Kutangaza wachezaji wa kuachwa/kusitisha mikataba ni kuanzia Juni 1 hadi 21 mwaka huu wakati kupitia majina na kutangaza pingamizi ni kati ya Julai 21-31 mwaka huu.
Kipindi cha pili cha uhamisho kitaanza Novemba 1 hadi 20 mwaka huu wakati usajili utaanza Novemba 1 hadi 30 mwaka huu. Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kutoka Julai 20 mwaka huu. Ngao ya Hisani kwa ajili ya ufunguzi wa msimu kwa mikoa yote itachezwa Agosti 13 mwaka huu wakati mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom utaanza Agosti 20 mwaka huu.
TFF tunawaomba wadau wote kuhakikisha wanapata kalenda hii ili waweze kupanga shughuli na mipango yao kwa kuizingatia.
Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF