AZAM YASHINDWA KUISHUSHA YANGA VPL

AZAM FC aka wanalambalamba leo wameshindwa kufurukuta mbele ya wakata miwa wa Mtibwa Sugar baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kupitia mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara uliofanyika kwenye uwanja wa Manungu Turiani mkoani Morogoro.

Bao la Mtibwa lilipachikwa na  Zubery Katwila akiunganisha krosi ya Juma Abdul aliyepanda kusaidia mashambulizi.
Kwa matokeo hayo, Azam imeshindwa kuishusha Yanga kutoka nafasi ya pili na kubaki na pinti zake 21, ikiwa sawa na Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara, Yanga.
Katika hatua nyingine,  Moro United imeifunga Ruvu Shooting bao 1-0 kupitia mechi iliyopigwa kwenye dimba la Chamazi ambapo Godfrey Wambura aliiandika timu yake bao hilo akiunganisha pasi ya Gaudance Mwaikimba.

Post a Comment

Previous Post Next Post