KAMPUNI ya usafirishaji ya SeaGull ambayo pia inamiliki Hoteli ya Kigomasha imejitokeza kudhamini Ligi kuu ya soka Visiwani Zanzibar.
Msemaji wa Chama cha soka Zanzibar (ZFA), Munir Zakaria alisema wamefurahishwa na uamuzi wa SeaGull Kampuni inayotoa huduma ya usafiri kati ya Dar es Salaam, Unguja na Pemba.
Alisema SeaGull wamekubali kuidhamini Ligi hiyo kwa jumla ya sh mil 41.5, ambapo itatoa jezi pea mbili kwa kila timu ambazo jumla yake ni sh mil 7, nauli kwa timu zote 12 zitakazoshiriki Ligi hiyo, jumla ikiwa sh mil 18.