RAIS wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia ‘Wazee
wa Ngwasuma’ Nyoshi El Saadat anatarajiwa kurejea nchini Ijumaa akitokea
nchini Uholanzi alipokwenda kuzifanyia ‘Mastering’ nyimbo
zao nne ambazo zitakuwemo kwenye albamu yao mpya zitakazokuwemo kwenye albamu yao mpya inayokwenda kwa jina la 'Chuki ya Nini' na kuzitaja nyimbo hizo ni pamoja na Otilia, Ndoa
ya Kisasa, Dai Chako Ulaumiwe na Fataki.
Mara baada ya kuwasili siku hiyo
atahudhuria onyesho la bendi hiyo litakalofanyika kwenye ukumbi wa Kijiji cha
Makumbusho, uliopo Kijitonyama jijini dar es Salaam ambalo litakuwa mahususi kwa ajili ya
kumkaribisha.
“Nawaomba mashabiki wa FM Academia mjitokeze kwa wingi
siku hiyo katika ukumbi wetu pale Makumbusho kwani pamoja na burudani toka kwa
bendi yenu pia nitakuja na mazawadi kutoka Uholanzi ambayo yote ni sehemu ya
kuwapa raha,”Alisema.