WAKATI tamasha maalum kwa vyombo vya habari ‘Media Day’
kwa mwaka 2012 likipangwa kufanyika
Machi 24 kwenye ufukwe wa Msasani, Kampuni ya bia Tanzania (TBL) imetoa shilingi mil.62.5 kwa
ajiliya kudhamini tamasha hilo.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Jamii na Sheria wa TBL
Steven Kilindo alisema kuwa wameamua kudhamini tamasha hilo kutokana na
kuthamini mchango wa waandishi wa habari katika biashara za kampuni yao.
“TBL itahakikisha bonanza la mwaka huu linafana na
litakuwa la aina yake kuanzia katika michezo, burudani, vinywaji na vyakula,
hivyo tunawaomba waandishi wajitokeze kwa wingi ili kuweza kubiridika pamoja na
kubadilishana mawazi,”Alisema Kilindo.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za
Michezo (TASWA) ambayo ndiyo waandaaji wa bonanza hilo Juma Pinto, pamoja na
kuishukuru TBL kwa udhamini huo aliiomba kutoishia kudhamini kwenye mabonanza
tu bali wafanye hivyo hata katika mafunzo mbalimbali yanayoaandaliwa na chama
hicho.
Kwa upande wake Katibu Msaidizi wa Taswa, George John
alisema kuwa tamasha hilo litashirikisha waandishi 1500 kutoka vyombo
mbalimbali vya habari ambapo kutakuwa na michezo mbalimbali itakayotangazwa
baadaye pamoja na burudani ya muziki