NI ajabu, lakini na kubali Gunners wako sawa. Thomas
Vermaelen alifunga bao la ushindi katika dakika ya 95 dhidi ya Newcastle, na
kupunguza tofauti ya pointi kati yake na Tottenham kuwa ni pointi moja tu. Tottenham
imo katika nafasi ya tatu, na Arsenal inashikilia nafasi ya nne.
Hatem Ben Arfa aliwawezesha Newcastle kupata bao la kwanza
katika mechi hiyo ya Jumatatu jioni kwa bao la chini kwa chini, lakini furaha
yao ilizimwa hata kabla ya dakika moja kumalizika.
Theo Walcott alimsukumia mpira Robin van Persie, na ambaye
alifunga bao lake la 33 msimu huu.
Mvutano ulizuka uwanjani baada ya kipenga cha mwisho,
kufuatia bao la Vermaelen ambalo liliingia wavuni huku mechi ikielekea
kumalizika, na mechi hiyo ikiwa ni ya nne ambayo Arsenal, baada ya kuachwa
nyuma, iliweza kujitahidi na kupata ushindi.
Ulikuwa ni ushindi wa kusisimua kwa mashabiki wa Arsenal,
timu ambayo imecheza vizuri sana hivi karibuni, hasa ikifikiriwa kwamba
majirani Spurs walikuwa na tofauti ya pointi 12 kati yao na Arsenal, kabla ya
mechi sita zilizopita.