KLABU ya REAC ya Hungarian ambayo inakabiliwa na kashfa ya
kupanga matokeo, imepata pigo baada ya Mkurugenzi wake, Robert Kutasi kudaiwa
kujiua.
Taarifa ya timu hiyo yenye maskani yake Budapest, imesema
leo kwamba Robert Kutasi alifariki Alhamisi. Taarifa ya Polisi ilisema
alijiruisha kutoka ghorofani. Alikuwa ana umri wa miaka 48.
Wachezaji sita wa REAC walipelekwa Polisi Jumanne kwa
kuhojiwa juu ya skendo ya kupanga matokeo, ambayo hadi sasa watu 25
wamekwishahojiwa.
Pamoja na wachezaji wa timu hiyo kufikishwa rupango, lakini
viongozi wa REAC hawahusishwi katika skendo hiyo.
Kutasi aliyekuwa kinara wa mapambano dhidi ya rushwa katika
soka ya Hungary, aliliambia gazeti la kila siku la Nemzeti Sport wiki hii
kwamba; “Maisha yangu yameisha” kwa sababu ya kesi.