Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo, Dk. Fenella Mukangala anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa
kuchangia timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kupitia Tigo
Pesa.
Uzinduzi huo wa akaunti
maalumu ya Twiga Stars kupitia mtandao wa Tigo utafanyika kesho (Machi 10 mwaka
huu) saa 5 kamili asubuhi Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam. Twiga Stars iko kwenye mashindano ya Kombe la Afrika kwa
Wanawake (AWC) ambapo Mei 26 mwaka huu itacheza na Ethiopia jijini Addis
Ababa.