MIAMBA
ya soka barani Asia, Australia
na Japan zinazoonekana ndizo zenye nguvu kwa sasa zimejikuta zikipangwa pamoja
katika ngwe ya mwisho ya kusaka tiketi ya kushiriki fainali zijazo za kombe la
Dunia mwaka 2014.
Katika
hafla ya upangaji wa makundi zilizofanyika makao makuu ya Shirikisho la soka
Asia (ASF) Malaysia , timu
hizo zimepangwa kwenye kundi B, kusaka tiketi za kushiriki fainali hizo
zitakazofanyika nchini Brazil .
Mbali
ya Australia na Japan, kundi
B litakuwa pia na timu za Iraq ,
Jordan na Oman .
Kwenye
kundi A kuna waliokwua wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002, Korea
Kusini, Iran, Lebanon, Uzbekistan na wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia mwaka
2022, Qatar.
Timu
mbili za juu kutoka kila kundi zitajikatia tiketi ya kushiriki fainali hizo,
wakati timu zitakazoshika nafasi ya tatu kutoka kila kundi zitalazimika kucheza
ili kupata timu ya tano itakayoliwakilisha bara hilo .
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na ASF, kinyang’anyiro hicho cha kusaka tiketi
hizo kinatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 3, 2012 na zitamalizika ifikapo Juni
18, 2013.