Siku tatu kabla ya kuwavaa Es Setif ya Algeria, kocha mkuu wa
Simba, Mserbia Milovan Cirkovic, amewapunguzia wachezaji wake vipindi vya
mazoezi, kutoka mara mbili hadi mara moja kwa siku.
Simba na Es Setif watakwaana jumapili katika mchezo wa kuwania kombe la Shirikisho (CAF) ambao utapigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Milovan amefanya hivyo ili kutochosha miili ya wachezaji wake ambapo kuanzia
jana watakuwa wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa jioni tu.
Aidha, Simba imejipanga vema kushinda mabao mengi zaidi, ili kujiweka katika mazingira
mazuri ya kushinda katika mechi ya marudiano na hatimaye kusonga mbele, huku
wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri, isipokuwa Juma Jabu ambaye anakabiliwa
na majeraha.
