SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF)
linatarajia kujaidili kauli ya kugomea wachezaji wake kuichezea timu ya Taifa
‘Taifa Stars’ iliyotolewa juzi na klabu ya soka ya Simba.
Simba kupitia kwa mwenyekiti
wake Alhaj Isamil Aden Rage alisema juzi kwamba watafikia hatua hiyo kutokana
na TFF kutothamini mchango wa vilabu vya
Ligi kuu ambavyo ndiyo chimbuko la Stars lakini badala yake imekuwa ikiwaonea
katika mapato.
Rage alitolea mfano wa
wachezaji wao waliokuwa wakiitumikia Stars kurudishwa siku mbili kabla ya mechi
yao ya kombe la shirikisho dhidi ya Kiyovu ya Rwanda na kusema kuwa kama TFF
ingekuwa inawajali ingeomba kusogezwa kwa mchezo huo.
Ofisa habari wa TFF Boniface
Wambura amesema leo kwamba kauli ya Rage si nzuri na inapaswa kukemewa
kwani Stars ni timu ya Taifa na si mali ya TFF,m hivyo watalijadili hilo kabla
ya kulitolea maamuzi.
Aidha, Wambura alisema TFF
imelazimika kuikata Simba mil.5 kama fidia ya uharibifu wa vbiti 152 uliofanywa
na mashabiki wakati wa mchezo wao dhidi ya Kiyovu jumapili iliyopita kutokana
na ukweli kwamba mchezo huo uliwahusu wao.