KLABU ya soka ya Simba kwa kushirikiana na jeshi la polisi juziwameendesha
zoezi la uvunjaji wa nyumba zilizojengwa katika eneo laUwanja wao huko Bunju
nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaj Ismail
Aden Rage alisema jana kwamba wavamizi hao walijenga nyumba tatu
ambazo zilikuwa katika hatua za mwisho wakati wakijua eneo hilo ni mali ya
Simba.
Alisema baada ya kuwauliza watu wanaodaiwa kuhusika na umiliki
wanyumba hizo kila mtu alijitetea anavyojua ambapo kuna mmoja
alidai
kuuziwa eneo hilo na mwingine alidai kuwa alipatiwa na babu
yake.
“Mimi nashangazwa na wavamizi hawa sijui wanajiamini nini…baada
ya kubaini uvamizi huo tulitaarifu polisi na wakafanya uchunguzi wao
na sisi tukatoa vithibitisho na juzi kuliendeshwa zoezi la uvunjaji
wa
nyumba hizo,”Alisema.
Rage alisema wakati wowote wataalamu wa kampuni
ya Petroland yanchini Uturuki wanatarajiwa kutua na kuanza mchakato wa
kuelekeaujenzi wa uwanja huo ambapo utakapokamilika utakuwa na uwezo
wa kuchukua mashabiki 60,000, pia utazungukwa na vitega
uchumi
vya aina mbalimbali..
TAMTHILIA YETU YA UWANJA WA KISASA WENYE MADUKA INAENDELEA,ADEN...NAMPENDA SANA KAKANGU YULE ANAWAPATIA SANA SIMBA...!
ReplyDeleteWATAALAM WANAKUJA KUANZA MCHAKATO WA KUELEKEA UJENZI...
CHANGA LA MACHO LA TV YA SIMBA KUMBE NI TV SHOW TUMEELEZWA NI MCHAKATO KUELEKEA SIMBA KUMILIKI TV YAKE,HII MIKAKATI NA MICHAKATO ADEN ITAKAMILIKA WAKATI MUDA WAKE WA KUKAA MADARAKANI
UMEKWISHA,NI STRATEGY TU YA KUITAWALA SIMBA KWA AMANI NA UTILIVU