BEKI wa klabu ya Yanga Chacha Marwa amefiwa na mtoto wake hivyo amelazimika
kurejea jijini Dar es Salaam ili kuungana na wanafamilia katika msiba huo.
Aidha, mamia ya watu wakiwemo
wanamichezo jana walijitokeza katika kanisa katoliki parokia ya Mtoni Kijichi
kwa ajili ya kuaga mwili wa aliyekuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji ya klabu ya
Yanga, Wakili Theonest Rutashoborwa.
Rutashoborwa ambaye alikuwa akimiliki kampuni ya Brilliance Law Chambers ya jijijini Dar es
Salaam alifariki usiku wa kuamkia Ijumaa
katika hospitali ya Aga Khan kutokana na kuugua shinikizo la damu na kisukari
anatarajiwa kuzikwa kesho katika kijiji cha Bukabaye kilicopo Bukoba mkoani
Kagera.
Aidha uongozi wa Yanga kupitia Mwenyekiti wake Lloyd
Nchunga umeelezwa kusikitishwa na kifo cha marehemu ambaye aliweza kuunganisha Wanayanga
ambapo klabu hiyo ilitoa ubani wa shilingi mil.1.5.