Na Mwandishi Wetu

MTANDAO wa wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa ibada maalum ya kumwombea marehemu Steven Kanumba itakayofanyika Jumapili Aprili 15,2012 kwenye ukumbi wao wa Ilala, Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Caasim Taalib alisema jana kuwa amewaomba wanachama wote wahudhurie ibada hiyo ambayo ni moja ya matukio ya mtandao huo katika kuwaombea wanachama waliofikwa na vifo akiwemo mwanachama wao Kanumba aliyeshiriki kwa ukamilifu, uadilifu na mchango mkubwa katika shirikisho hilo katika harakati za kujikomboa kiuchumi.
Caasim alisema Kanumba ambaye alikuwa mwanachama wa SHIWATA alikuwa mchapakazi, mpenda maendeleo na aliyewahi kushiriki kikamilifu katika kutafuta mashamba na maeneo ya makazi ambako alikwenda Bagamoyo, Kisarawe na hatimaye kufanikiwa kupata eneo wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani, katika mashamba hayo wanachama zaidi ya 1,000 wamefanikiwa kupata maeneo ya makazi marehemu Kanumba akiwa mmojawapo.
Alisema SHIWATA inakusudia kujenga makumbusho makubwa ya wasanii waliofariki wakiwa katika harakati za kuendeleza kazi za wasanii katika kijiji cha Mwanzega.
"Katika makumbusho hayo pia zitawekwa kumbukumbu za kazi za sanaa ikiwemo ya Waziri Mkuu wa zamani marehemu, rashida Kawawa aliyeacheza sinema ya Muhogo Mchungu pamoja na wengine kama marehemu Fundi Saidi (Mzee Kipara),wasanii 13 wa Five Stars na Kanumba"alisema Bw. Caasim.
Alisema SHIWATA pia inakusudia kuandaa mashindano ya sanaa ya vikundi mbalimbali wakianzia mkoa wa Dar es salaam, mashindano kama hayo yaliwahi kufanyika mwaka 2003 kati ya vikundi vya Kaole,Splendid, Savanna, Nyota Academia,Mambo hayo, Kidedea,Black Eagle na kuibua vipaji mbalimbali akiwemo Cheni, Muhogo Mchungu na marehemu Kanumba.
Lengo la mashindano hayo ni kuinua vipaji vya wasabii wa bongo Flava, Sarakasi, filamu,ngoma, taarabu,muziki wa dansi,%2