KOCHA mkuu wa timu ya Taifa Taifa Stars amewataka wachezaji wake kutohofia nyota waliopo katika kikosi cha Ivory Coast kwani hawana tofouti na wao.
Stars na Ivory Coast watkawaana Juni 2,
mjini Abidjan, katika mechi ya kuwania kucheza fainali za kombe la
dunia ambapo kikosi cha Ivory Coast kinawachezaji wanaosakata soka la kulipwa barani Ulaya wakiwemo Didier Drogba, . Yaya Toure na
Solomon Kalou na wengineo.
Kim alisema wanaiheshimu Ivory Coast kama moja ya timu yenye wachezaji wazuri lakini hawaihofii kwani wachezaji wa Stars pia ni wazuri ingawa wanatofaitiana vitu vidogo vidogo tu.
Kocha huyo aliwataka wachezaji wake kupambana kadiri wawezavyo katika mchezo huo kwani ndio
siri ya ushindi na mafanikio ya timu yoyote.