Dar es Salaam, Jumatatu Mei 28, 2012…Airtel Tanzania leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa
timu za shule za sekondari 24 zitakazoshiriki kwenye michuano ya vijana wenye
umri chini ya miaka 17 maarufu kama Airtel Rising Stars ambayo inatarajiwa kuanza
kutimua vumbi Jumatano, Mei 30, ngazi ya Mkoa.
Shule
zitakazoshiriki kwenye michuano hiyo ni zile zilizofanya vyema kwenye michuano
ya shule za sekondari (UMISSETA), ambazo ni Lindi sekondari, Mpunyule na Nkowe
zote za Mkoa wa Lindi, Southern Highland ,
Mbeya Day na Wenda Sekondari kutoka Mbeya.
Nyingine
ni Mbande Sekondari, Kurasini na Kiravi (Temeke), Airwing, Benjamini Mkapa na
Msogola Sekondari (Ilala), Twiga Sekondari, Goba na Makongo Sekondari
(Kinondoni), Sinoni, Kaloleni na Bishop Durning (Arusha).
Timu
hizo zote zimethibitisha ushiriki wao na kuahidi kufanya vizuri ili kushinda
mechi zao. Mechi za mikoa zitatumika kuchangua timu kombaini zitakazowakilisha mikoa
kwenye mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa yatakayoanza Juni 9
mpaka Juni 17 Jijini Dar es Salaam.
Katika
hatua nyingine, Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) leo imetoa ratiba
ya michuano ya ARS ngazi ya mkoa kwa timu 24. Ratiba hiyo inaonyesha kuwa shule
ya …….itacheza na ……….kwenye ufunguzi wa Kinondoni, ………….na…………..kutoka Ilala
zitapambana kwenye mechi ya ufunguzi. …………. Itacheza na …………kutoka Temeke
huku………..ikicheza na ………….kutoka Arusha.
Kutoka
Mbeya, mechi ya ufunguzi itakuwa baina ya ………….na ……………….kwenye uwanja
wa…………Mkoa wa Lindi shule ya ……….itacheza na ……………..kwenye ufunguzi huo.
Wakati
timu za wavulana zikatarajiwa kushindana kwenye ngazi ya mkoa ili kuchanguliwa
kucheza michuano ya Taifa, timu moja kutoka kila Mkoa itafuzu moja kwa moja na
kufanya timu zitakazoshiriki ngazi ya taifa kuwa 12, sita za wavulana na sita
wasichana.
Akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar
es Salaam leo, Meneja Masoko na Matangazo Airtel Tanzania Rahma
Mwapachu alisema Airtel inajivunia ushirika wake na moja ya Klabu kubwa duniani
– Machester United, kuinua kiwango cha mpira wa miguu nchini Tanzania na
Afrika.
‘Tunaamini ya kuwa kwa ushirikiano wetu na
Manchester United na TFF tutakuza kwa kiasi kikubwa kiwango cha mpira wa miguu
hapa nchini Tanzania .
Tunaamini vijana wakiandaliwa vizuri wanaweza’.
Mwapachu
alishukuru Wizara ya Habari, Vijana, Utamanduni na Michezo kwa ushirikiano wanaotoa
ili kukuza mpira hapa nchini.
Airtel
Rising Stars ni mpango kabambe wa Afrika nzima ambao ni kuibua na kukuza vipaji
vya wanasoka wanaochipukia, wavulana na wasichana wenye umri wa miaka chini ya
kumi na saba ambao watapata muda muafaka wa kuonyesha vipaji vyao na kukutana
na waatalum wa mpira wa miguu na kupata mafunzo zaidi hivyo kukuza vipaji vyao.
Mwaka
jana, Klabu ya Manchester United ilitoa walimu wake wa soka la vijana kufundisha
kliniki za soka za kimataifa zilizofanyika Tanzania ,
Afrika Kusini na Gabon
ambapo walishiriki walipata nafasi ya kufundisha jinsi ya kucheza mpira wa
miguu kwa mtindo wa Manchester
United.
Kliniki
ya aina hiyo itafanyika Jijini Nairobi Agosti mwaka huu kwa nchi zinazozungumza
Kingereza Tanzania
ikiwemo. Nairobi
pia itakuwa mwenyeji wa mashindano ya Airtel Rising Stars inter-continental
ambayo itashirikisha nchi 14 ambapo Airtel inafanya biashara. Tanzania
itawakilishwa na mshindi wa fainali za taifa pamoja na wachezaji sita bora,
watatu wavulana na watatu wasichana.