WAKATI kamati ya uchaguzi ya
Yanga ikitupilia mbali pingamizi la mwanachama Abeid Falcon, kamati hiyo kesho inatarajiwa kusikiliza pingamizi walizowekewa wagombea wa nafasi mbalimbali za
uongozi katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Julai 15.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jaji John Mkwakwa (pichani) amesema wametupilia
mbali pingamizi la Falcon kutokana na kutokuwa na mashiko yoyote.
Alisema kamati yake
inashangazwa na Falcon kupinga katiba ya klabu hiyo ambayo aliwahi kugombea
uenyekiti mwaka 2010 akitumia katiba ya mwaka huo ambayo iliwasilishwa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Juni 17, 2010 na kusajiliwa kwa msajili wa
vyma vya michezo.
Aliongeza kuwa kamati yao
inaendelea na mchakato wa uchaguzi ambapo leo itasikiliza pingamizi walilowekewa
wagombea Yusuf Manji (mwenyekiti), Stanley Yono Kevela, Ali Mayay na Clement
Sanga wanaowania nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Mkwawa alisema baada ya zoezi
hilo wanatarajiwa kuwafanyia usaili wagombea Juni 22 na 23, hivyo amewaomba
wanachama kufuata taratibu zilizowekwa katika mchakato huo.
“Tufanya kazi kwa miongozo
iliyowekwa na si kwa shinikizo la mtu au kikundi cha watu, hivyo tunawaomba
wanachama na kufuata taratibu hizo,”alisema Jaji Mkwawa.