KLABU ya soka ya Yanga mevunja mkataba wa mshambuliaji wake Mzambia Davies Mwape.
Katibu
mkuu wa klabu ya Yanga Mwesiga Selestine amesema leo kwamba, Mwape ambaye
alibakiza miezi sita ya kutumikia mkataba wake amelipwa stahiki zake zote.
“Tumevunja
rasmi mkataba na Mwape ambao ulibakiza miezi sita…tayari tunmeshamwandikia
barua yake na kumpa stahiki zake zote,”alisema Mwesiga.
Katika
hatua nyingine, kikosi cha Yanga chini ya kocha msaidizi Fred Felix Minziro
kimeanza mazoezi leokwenye uwanja wa Kaunda ikiwa ni maadalizi ya michuano ya
kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi julai 11 jijini Dar es
Salaam.
Kupitia mazoezi hayo
wachezaji 10 wameripoti wakiwemo Athuman Iddi ‘Chuji’, Godfrey Taita, Oscar
Josua, Rashid Idrissa, Yaw Berko, Kenneth Asamoah na Ibrahim Job, huku Nizar
Khalfan na Mwape wakishindwa kufanya kutokana na kuwa na maumivu