MANJI
YONO
WAKATI kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la soka
Tanzania (TFF) inatarajiwa kuketi Julai 2 kwa ajili ya kupitia pingamizi zilizowasilishwa
kwa wagombea uongozi wa klabu ya Yanga, wagombea wawili Yusuf Manji na Stanley Yono Kevela wamewekewa
pingamizi.
Klabu ya Yanga inatarajiwa
kufanya uchaguzi mdogo julai 15 jijini Dar es Salaam ili kuziba nafasi za
baadhi ya viongozi waliojiuzulu akiwemo mwenyekiti Lloyd Nchunga.
Mjumbe wa kamati hiyo iliyo chini ya mwenyekiti wake Deogratius
Lyatto, Salum Mbwezeleni alisema kwamba kamati yake itapitia pingamizi hizo kwa
kusikiliza wapingaji na waliopingwa na kisha kutoa maamuzi.
Hata hivyo, Mbwezeleni hakuweza kutoa ufafanuzi wa pingamizi wa wagombea hao Manji
(Uenyekiti) na Kevela (Makamu Mwenyekiti, Ujumbe) kwa madai kuwa bado
hajapitia maelezo yaliyowasilishwa na waliopinga.
“Ninachoweza kusema kwa sasa
ni kuwa kamati itakutana Julai 2 na kuwasikiliza wahusika wote na kisha tutatoa
maamuzi ili majina yaweze kutangazwa na wagombea waanze kampeni zao,”alisema.
Kamati ya uchaguzi ya Yanga chini
ya mwenyekiti wake Jaji Mstaafu John Mkwawa wiki iliyopita ilitawataja
waliopitishwa katika ujumbe ni pamoja na Jumanne Mwamenywa,Edgar Fongo, Beda
Tindwa, Ramadhan Said,Omary A. Ndula, Shaban Katwila,Ramadhan Y. Kampira,Lameck
Nyambaya na Peter H. Haule.
Wengine ni Justine S. Baruti,Abdalah A. Mbaraka, Kevela,Mosess
K. Valentino,Aaron Nyanda,George M. Manyama.Abdalah Sharia Ameir,Jamal Kisongo
na Gaudiusus Ishengoma.
Huku wanaowania nafasi ya
Makamu Mwenyekiti ni Ayoub Nyenze, Kevela na Clement A. Sanga, wakati Jonh Paul
Jambele, Manji, Edgar W. Chibula na Sarah Ramadhan wameomba katika nafasi ya
uenyekiti,”alisema.
Uchaguzi huo ambao umepangwa kufanyika Julai 15 mwaka
huu, umelenga kuziba nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanne
wa kamati ya Utendaji ambao walijiunzulu.