Sanga,
amewasihi wanachama wa klabu hiyo kumpatia kura katika uchaguzi huo ilii aweze
kushirikiana na wengine kuijenga Yanga imara kisoka na kiuchumi.
Anasema kama atapewa ridhaa ya kuingia madarakani,
atajitahidi kupigania umoja miongoni mwa viongozi na wanachama.
Alisema
licha ya kila mwanachama kutaka mafanikio ya soka na kiuchumi, lakini
mshikamano ndio nyenzo muhimu ya kufikiwa kwa mafanikio hayo.
Mgombea
huyo alisema ataimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama kuanzia kwa
vijana hadi wazee bila kuvisahau vikundi vya uhamasishaji ambavyo licha ya
kufanya kazi kubwa, vimekuwa havipewi heshima yake.
Sanga
anabainisha kwamba kingine, atakachopigania kwa kushirikiana na viongozi
wengine kama atashinda, ni uwekezaji kwenye soka ya vijana kwani huo ndio
msingi wa mafanikio ya soka kote duniani.
Kuhusu
uchumi wa klabu, ni kuhakikisha Yanga inakuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato
kama uwanja na jina lake kutumika kibishara zaidi tofauti na ilivyo sasa.
Aidha,
atajitahidi kuwawezesha wanachama kiuchumi kwa kuanzisha Mfuko wa Akiba na
Mikopo kwa Wanachama (Saccos) ambao utakuwa ukitoa mikopo kupitia matawi yao.
Juu ya
uendeshaji wa klabu, Sanga alisema akishinda, ataunda Idara za Uhasibu, Masoko,
Sheria na Habari, Mawasiliano na
Uhusiano kwa lengo la kurahisisha utendaji
kazi.
Sanga
alisema, jambo jingine ni uimarishaji wa
matawi ya klabu hiyo
ikiwemo kuwaelimisha wanachama umuhimu wa kuichangia klabu yao.
Alisema,
kuwepo kwa msingi imara kisoka na Kiuchumi,
Yanga itaweza kuwa na kikosi imara Dimbani,
hivyo kufanya vema kwenye michuanoya kitaifa
na kimataifa.
Hata hivyo,
akasisitiza suala la uvumilivu wa wanachama dhidi ya
uongozi kwani mafanikio hujenga kupitia mikakati ya muda
mfupi, muda wa kati na muda mrefu.
Sanga
alisema kama akipata ridhaa ya kuingia madarakani, atashirikiana na wenzake
kuangalia pia uwezekano wa kufanyia marekebisho katiba ili iweze kuendana na
wakati.
Kwa
mazingira hayo, Sanga amewasihi wanachama wa klabu hiyo
kuutumia vizuri muda wao wa kutoka nyumbani hadi ukumbini kwa kumchagua yeye na
wengine kwa ajili ya
maendeleo ya klabu hiyo kisoka na kiuchumi.