MIMI JOHN PAUL JAMBELE MGOMBEA WA NAFASI YA MWENYEKITI WA KLABU YA YANGA KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA KUJAZA NAFASI ZILIZO ACHWA WAZI NA BAADHI YA VIONGOZI WALIOJIUZULU UTAKAOFANYIKA SIKU YA JUMAPILI YA TAREHE 15/07/2012.
NIMELENGA KATIKA KUHAKIKSIHA NINASHIRIKIANA NA “WANAYANGA” WOTE NCHINI TANZANIA NA SEHEMU NYINGINE POPOTE DUNIANI KATIKA KUIFANYA KLABU HII IJITEGEMEE YENYEWE KIMAPATO NA KUPUNGUZA KWA KIASI KIKUBWA (80%) KAMA SIO KUONDOA KABISA TABIA YA KUWA TEGEMEZI WAKTI INA RASILIMALI ZA KILA AINA ZINAZOWEZA KUIFANYA IWE NA MAFANIKIO MAKUBWA SANA KATIKA KUJIENDESHA YENYEWE KIUCHUMI.
ENDAPO WANACHAMA WA YANGA WATANIPA KURA ZA USHINDI DHIDI YA WAGOMEA WENZANGU, JAMBO LA KWANZA NITAANZA NA KUTENGENEZA “MIFUMO” NDANI YA KLABU KATIKA NYANJA ZA “UTAWALA NA UONGOZI”, “NIDHAMU KATIKA MASWALA YA UTAWALA WA FEDHA”, “MIFUMO YA KUMBUKUMBU PAMOJA NA MITANDAO YA KELEKTRONIA” NA SHERIA NA KANUNIZA MANUNUZI.
KATIKA NYANJA NILIZOTAJA HAPO AWALI SHERIA, KANUNI NA MIONGOZO MBALIMBALI ITAWEKWA KATIKA MAANDISHI, HIVYO KUFANYA UTENDAJI WA SHUGHULI ZA KLABU SIKU HADI SIKU KUWA RAHISI, WENYE KUELEWEKA NA KUJENGA UWEZO KWA VIONGOZI WANAOPATA FURSA YA KUINGIA MADARAKANI WAWEZE KUIONGOZA YANGA KWA MAFANIKIO AMBAYO YANATARAJIWA NA WANAYANGA WOTE.
KATIKA KUELEKEA KWENYE KUJITEGEMEA NITAWASHIRIKISHA WANAYANGA WOTE AMBAO WANAKADIRIA KUFIKIA ZAIDI YA MILIONI KUMI NDANI YA TANZANIA NA KFUANYA SENSA YA HARAKA KUWAPATA KATI YA MILIONI HADI MILIONI TATU AMBAO WATAKUWA TAYARI KUTOA NAMBA ZAO ZA SIMU ZILIZOSAJILIWA NA KUWA TAYARI KUICHANGIA KLABU KWA KUKUBALI KUKATWA KATI YA SHILINGI 250/= HADI SHILINGI 500/= KWA WIKI ILI KLABU IWEZE KUPATA MAPATO TOKA SIMU ZAO.
HATUA INAYOFUATA NIKUTANGAZA ZABUNI KWA KAMPUNI ITAKAYOKUWA TAYARI KUSIMAMIA ZOEZI LA KUIKUSANYIA NA KUWEKA KWENYE AKAUNTI MAALUM YANGA, FEDHA TOKA KWA WANAYANGA WOTE NCHINI KOTE.
Jambele akimwaga sera mbele ya Sports lady, Dina Ismail
KLABU ITAHITAJI KUPATA KATI YA SHILINGI MILIONI 150 HADI 200 KWA WIKI AMBAPO IKIWA WANAYANGA MILIONI TATU WATAUMIKA BASI KLA MMOJA ATACHANGIA SHILINGI 50/= KWA WIKI NA YANGA KUPATA SHILINGI MILIONI 150/= AMBAZO KWA MWEZI ITAKUWA NI SHILINGI MILIONI 600. FEDHA NYINGINE KWENYE MAKATO HAYO ZITABAKI KWENYE KAMPUNI HUSIKA KWA AJILI YA KULIPIA KODI NA GHARAMA NYINGINE ZA UENDESHAJI.
KWA FEDHA HIZI TU AMBAZO KULINGANA NA TEKNOLOJIA YA KISASA ILIYOPO NI RAHISI SANA KUPATIKANA BILA KUJALI ENEO LA KIJIOGRAFIA ALIPO MWANAYANGA ZINAWEZA KUSAIDIA SANA KWA KLABU KUJIENDESHA YENYEWE, KULIPA MADENI YALIYOPO PAMOJA NA KUKAMILISHA MIPANGO MBALIMBALI YA MAENDELEO YA KLABU KAMA VILE UJENZI WA UWANJA WA KISASA, MAJENGO YA KISASA YA KIBIASHARA N.K.
KWA MFANO KAMA YANGA ITATUMIA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 200 KWA MWEZI KWA AJILI YA MATUMIZI YA KAWAIDA, BASI ITABAKIWA NA BAKAA YA SHILINGI MILIONI 400 KILA MWEZI KIASI AMBACHO KWA MWAKA KLABU ITAKUWA INA BAKAA YA SHILINGI BILIONI 4.8 AIDHA, KLABU ITATUMIA “LOGO” (NEMBO) YAKE KATIKA KUTANGAZA ZABUNI KWA KAMPUNI AMBAYO IKO TAYARI KUTENGENEZA/KUUZA VIFAA MBALIMBALI KWA KUTUMIA NEMBO HII KWA MFANO FULANA, BUKTA, KOFIA, SKAFU, STICKERS, TRUCKSUITS, KANGA, MIAVULI, MABEGI, KAVA ZA MATAIRI YA GARI N.K NA KUINGIA NAYO MKATABA WA MWAKA MMOJA AMBAPO VIFAA VYOTE HIVI SISI TUTAVIITA NI “SETI” MOJA.
KAMPUNI HII TUAITAKA IWE NA UWEZO WA KUTENGENEZA SETI MILIONI MOJA KWA MWAKA NA SISI YANGA TUTAHITAJI SHILINGI 3,000/= (ELFU TATU TU) KWA SETI AMBAPO KLABU ITAJIINGIZIA JUMLA YA SHILINGI BILIONI 3 KWA MWAKA. KAMPUNI ITAPEWA KIBALI CHA KUMCHUKULIA HATUA ZA KISHERIA MTU YEYOTE ATAKAYEKUTWA ANAUZA VIFAA HIVI NDANI YA MWAKA HUSIKA BILA YA KIBALI TOKA KWAO. JUMLA YA BAKAA KWENYE AKAUNTI YA KLABU ITAKUWA NI SHILINGI BILIONI 7.8.
HII NI MIPANGO YA
MUDA MFUPI WA KATI YA MIEZI MITATU NA SITA BAADA YA KUCHAGULIWA, NAJUA ZIPO
CHANGAMOTO AMBAZO WANAYANGA WENGI ZINAWAKWAZA JUU YA UDHIBITI WA MAPATO HAYA NA
MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA ZOTE. NAPENDA
KUWAHAKIKISHIA WANAYANGA WOTE KUWA NITAITUMIA TAALUMA YANGU KATIKA KUHAKIKISHA
KUWA NIDHAMU NA UWAZI KATIKA MAPATO YA KLABU VINAKUWEPO KWA KIWANGO CHA HALI YA
JUU SANA NA YAFUATAYO NITAYAFANYA:-
1.
KWANZA KABISA NITAHAKIKISHA KLABU INAKUWA NA AKAUNTI NNE.
(i)
AKAUNTI YA KWANZA
NI AKAUNTI MAALUM (SPECIAL ACCOUNT)