MSHAMBULIAJI wa zamani wa Chelsea Nicolas Anelka amevunja ukimya kuhusiana na
uvumi ulioenezwa kwamba ana mpango wa kurejea England
na kusema kwamba atatundika daruga akiwa katika klabu yake ya sasa ya Shanghai
Shenhua ya China .
Hivi karibuni kulikuwepo na taarifa kwamba nyota huyo mwenye
miaka 33 amekuwa akiwaniwa na klabu zinazoshiriki ligi kuu ya England QPR na West Ham.
Anelka alisaini
mkataba wa miaka miwili na Shenhua mwezi
Desemba mwaka 2011, ambapo kwa sasa timu hiyo inashika nafasi ya 13 katika ligi kuu ya China.