MANJI AKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI
UCHAGUZI wa Klabu ya Yanga jana uliingia dosari baada ya Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti, Francis Mponjoli Kifukwe kutangaza kujitoa katika uchaguzi huo baada ya muonekano wa hujuma dhidi kutoka Kamati ya Uchaguzi ya Yanga.
Kifukwe alifikia hatua hiyo wakati alipokuwa akijieleza baada ya kujieleza mgombea, Edgar Chibura ambako alieleza kwamba mara nyingi amesingiziwa kwamba yeye ndio mtuhumiwa wa mabasi ya Yanga ambayo walinunua wakati wa uongozi wake na Tarimba Abbas.
Kifukwe alisema nilifikiri muda wa kampeni umekwisha tangu juzi ambako hadi jana katika uchaguzi ulikuwa ukiendelea jambo lililosababisha yeye kujiuzulu ambako alikosa cha kueleza zaidi lakini alitoa kauli kwamba mnyonge mnyongeni haki yake mpeni na mtoto akililia wembe mpe na kutoa kauli ya kujizulu.
Baada ya hatua ya kujitoa kwa Kifukwe ukumbi wa PTA ulizima na kuzua tafrani za hapa na pale baada ya Kifukwe kutaka kuondoka baada ya kutoa kauli hiyo hali iliyosababisha Naibu Waziri wa Hbari Utamaduni na Michezo Joel Nkaya Bendera kuingilia kati.
Wakati tafrani hiyo ikirindima ukumbini hapo baadha ya wanachama walipiga kelele za kueleza hakuna uchaguzi, ikawa fujo ukumbi mzima wengine wanadai mtoto wa rasi ndio ameharibu hivyo aongoze yeye kwani hana mamlaka na Yanga na wengine walieleza kwamba Kifukwe ameona hatapata ndio maana amejitoa.
Muingiliano wa kauli hizo ulisababisha Bendera atoe tamko kwamba ahatoondoka hadi hali ya mambo ikae sawa ingawa alikuwa na nia ya kuondoka kwa ajili ya majukumu mengine.
Waziri Bendera alialeza kwamba pamoja na Kifukwe kujitoa katika kinyang'anyiro hicho lakini hakufuata taratibu ilitakiwa kama alikuwa na nia ya kujitoa angefuata taratibu na si kufanya kama alivyofanya.
Kabla ya hayo kutokea Mdhamini wa Yanga, Yusuf Mehboob Manji aliyefika ukumbini hapo mapema akawa amekaa katika meza kuu akizungumza na baadhi ya wagombea waliofika katika uchaguzi huo.
Pamoja na Kifukwe kuzuiliwa na Bendera kutoondoka lakini alipata upenyo na kutoroka hali ambayo ilisababisha Manji kurejea tena ukumbini hapo baada ya kupigiwa simu kwamba hali ya hewa ukumbini hapo imeharibika.
Awali Manji aliondoka wakati Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Ridhiwani Kikwete alipokuwa akiwapa nasaha wanachama ambazo zilisababisha kuondoka kwake.
Baada ya kurejea ukumbini hapo Manji ambaye alimpigia simu Kifukwe warejee pamoja ambako baada ya kufika ukumbini hapo, Manji aliwaita wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na kuwaleza kwamba yoyote atakayechaguliwa kuwa Mwenyekiti ampendekeze Kifukwe kuwa mjumbe wa baraza la wadhamini.
Manji alisema Kifukwe akipendekezwa kuwa mjumbe wa baraza la wadhamini akubali ombi hilo ili kuendeleza umoja na mshikamano.
Manji awali alieleza kwamba aliondoka ukumbini hapo kwa sababu yeye si mpiga kura na baada ya kusikia Kifukwe amejitoa akarudi kurudisha amani na utulivu ndani ya Yanga.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Ridhiwani Kikwete katika taarifa yake ya kufungua mkutano alieleza kwamba viongozi watakaopatikana hawatawaridisha walipotoka na kuwaleza kwamba akawaeleza kwamba nderemo hizo zisiwe vilio kwa miaka minne.
Ridhiwani alisema wanaYanga wasiwachague viongozi ambao si waadilifu ambao wanaonekana ni wababaishaji ambao wanaweza kuirudiaha Yanga katika miaka iliyopita, kauli ambazo zilieonekana kama ni kumsema Kifukwe hali ambatyo iliyosabisha Manji kuondoka na Kifukwe kujitoa katika kinyang'anyiro.
Naye Mgeni rasmi katika uchaguzi huo, Joekl Bendera aliwaleza wana Yanga kuwa makini katika kuchagua na hata kama wameshawishiwa kiasi gani akawaambia akili za kuambiwa wachanganye na za kwao.
Bendera alisema pia sumu haionjwi kwani ukijaribu kuonja utakufa ambako alitoa kauli kuwa hawataki vongozi wababaishaji na mamluki, hawakai vikao na wanachama wabadhirifu wasiotoa taarifa za mapato na matumizi.
Bendera alisema wanataka viongozi makini na wanaoelewa katiba ya Yanga na kuachana na ubabaishaji.
Wanachama waliopiga kura ni 3517 ambako zoezi la kura lilifanyika katika hali isiyosalama kwa sababu wapiga kura walikuwa wakizurura na kura hadi nje ya ukumbi na si utaratibu uliozoeleka wa kupiga kura katika vibox ambavyo inakuwa siri lakini si.
Akitangaza kumaliza muda wake aliyekuwa Mwenyekiti Imani Madega alisema yeye si malaika ni binaadama kuna makosa ambayo aliwafanyia wana Yanga aliomba msamaha ambako alieleza kwamba ingawa kuna mabaya aliyoyafanya pia kuna mazuri aliyoyafanya aliomba yapokelewe.
Madega alitangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Chalinze ambako alieleza kwamba leo anakwenda kuchukua fomu za kuwanua ubunge katika jimbo hilo.
Ashubuhi wakati wanachama wakijiandikisha kulikuwa na misururu ambako wanachama waliwasili ukumbini hapo makundi kwa makundi.
Alipowasili Mgombea wa Makamu Mwenyekiti Davis Mosha alifika ukumbini hapo na 'maboncer' waliovalia suti nyeusi na miwani nyeusi na kuzunguka nao kila mahali.