WAWAKILISHI wa Tanzania Simba leo wana kibaruani kigumu watakapovaana
na timu ya Es Setif katika mchezo wa kuwania Kombe la Shirikisho mechi
itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Simba iliyopo chini ya kocha Mserbia Milovan Cikovic, ina kazi
kubwa ya kuhakikisha inafanya vizuri katika mchezo huo.
Wawakilishi hao wanaingia Uwanjani ikiwa na lengo la
kuifunga timu hiyo zaidi ya mabao 3-0 ili waweze kujiweka katika mazingira
mazuri katika kuendelea na mashindano.
Endapo Simba itashindwa kuifunga timu hiyo ya waarabu
itakuwa imejiweka pabaya katika kuendelea na mashindano hayo kwakuwa itakuwa na
mchezo mwingine wa ugenini.
Mchezo huo utaanza saa 10,alasiri ambapo waarabu hao
wamekuwa wakifanya mazoezi mchana kwa ajili ya kutaka kuizoea hali ya hewa.