LLOYD NCHUNGA
LLOYD Nchunga ametangazwa kuwa mwenyekiti mpya wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam atakayeongoza kwa kipindi cha miaka minne ijayo baada ya kuzoa kura 1437 na kuwaangusha wenzake wanne.
Akitangaza matokeo hayo jana, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Ridhiwani Kikwete alimtangaza Davis Mosha kuwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga aliyezoa kura 2142 na mpinzani wake Costantine Maligo aliambulia kura 55 na kura 23 ziliharibika kati ya kura 2491.
Wapinzani wa Nchunga ni pamoja na Francis Kifukwe aliyepata kura 370, Mbaraka Igangula alipata kura 305, Abedi Falcon alipata kura 301 na Edgar Chibura aliambulia kura 65 katika kura 2220 zilizopigwa ambako 23 kati ya hizo ziliharibika.
MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI YA YANGA, RIDHWAN KIKWETE AKITANGAZA MATOKEO LEO ASUBUHI, KULIA NI MFADHILI WA KLABU HIYO, YUSUF MANJI
Kikwete pia alitangaza majina ya wajumbe nane wa Kamati ya Utendaji ya Yanga walioongozwa na Ally Mayai Tembele aliyezoa kura 1734 aliyefuatiwa na Mzee Yusufu aliyepata kura 1517, Sara Ramadhani alipata kura 1500, Tito Osoro alipata kura 1460, Mohamed Bhinda alipata kura 1458, Charles Mgondo alipata kura 1300, Salum Rupia alipata kura 1231 na Theonest Rutashoborwa alipata kura 1225.
Baada ya kutangazwa matokeo hayo Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Davis Mosha aliyemwakilisha Mwenyekiti Nchunga ambaye hakuwepo wakati wa kutangaza matokeo alisema pamoja na uchaguzi huo kufanyika kuanzia juzi ni mojawapo ya upendo wa wanachama.
MAKAMU MWENYEKITI, DAVIS MOSHA AKITOA SHUKURANI KWA WANACHAMA
Mosha alisema baada ya kutangazwa jana walianza kazi rasmi kuanzia jana ambako alieleza ushirikiano uanze na makundi yavunjwe kwa kuwa nia ya Yanga ni umoja.
Aidha Mosha alisema matatizo yaliyojitokeza watayarekebisha ambako watashirikiana na walioshindwa katika kinyang’anyiro hicho ambako inawezekana wakawachukua katika uongozi huo.
Mdhamini wa Yanga, Yusufu Manji alitoa pongezi kwa wana Yanga kwa kazi nzuri ya kidemokrasia ambako alitoa rai kwa viongozi waliochaguliwa kuheshimu hatua ya wanachama na kuwaomba wasiwaangushe.
BAADHI YA WAJUMBE WALIOCHAGULIWA
SARAH RAMADHAN
ALLY MAYAI TEMBELE
CHARLES MUGONDO
THEOFRID RUTASHOBORWA
SALIM RUPIA
MZEE YUSSUF
MOHAMMED BHINDA