TENGA AKIMPA MKONO WA KWAHERI MWAKALEBELA
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeanza mchakato wa kumsaka katibu mkuu mpya baada ya aliyekuwepo, Frederick Mwakalebela kumaliza muda wake tangu juni 30.
Rais wa TFF Leodger Tenga alisema kamati ya utendaji itaketi jumamosi kwa ajili ya kujadili jinsi gani ya kumopata mbadala wa Mwakalebela.
Tenga alimpongeza Mwakalebela kutokana na kuonyesha ufanisi katika kipindi chake hivyo anamtakia kila la heri katika harakati zake za kisiasa.
Hivi karibuni Mwakalebela ametangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo la Iringa Mjini kupitia tiketi ya Cahama cha Mapinduzi (CCM).
Naye Mwakalebela aliwashukuru wadau wate wa soka ambao amekuwa akifanya nao kazi kwa kipnjdi chote cha uongozi wake, pia wadhamini wake katika medani ya siasa na kuwataka wamuombee dua katika hilo ili aweze kufanikishawakiwemo wadhamini alitoa wito kumuombea dua njema katika kinyang’anyiro hicho.