MJUMBE WA KAMATI YA UCHAGUZI YA YANGA,
PHILEMON NTAHILAJA AKIONYESHA WAANDISHI WA HABARI KADI ITAKAYOTUMIKA KATIKA UCHAGUZI WA YANGA UNAOTARAJIA KUFANYIKA JUMAPILI
KAMATI ya uchaguzi ya klabu ya Yanga chini ya Mwenyekiti wake Jaji John Mkwawa, hakutakuwa na zoezi la uhakiki wa wanachama katika uchaguzi huo na badala yake watapewa namba maalumu ambazo zitawawezesha kupiga kura.
Kwa mujibu wa mjumbe wa kamati hiyo, Philemon Ntahilaje, hatua hiyo inatokana na wanachama wote kuwa hai kwa miaka yote miwili, hivyo kuorodheshana, itakuwa ni kupoteza muda bure.
Alisema kadi zitakazotumika ni zile zilizotolewa mwaka 2007/ 2008 na kulipiwa na mfadhili wa klabu hiyo, Yussuf Manji.
Kuhusu maandalizi, alisema yamekamlikka na kwamba uchaguzi huo utaanza saa mbili kamili asubuhi kwani lengo ni kazi hiyo kwisha mapema.
JANE JOHN WA TBC 1
WAPIGA PICHA TOKA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI WAKIWAJIBIKA