MADEGA AKIMKABIDHI NCHUNGA KATIBA YA YANGA
MJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI TITO OSORO, NCHUNGA NA MADEGA
UONGOZI wa zamani wa klabu ya Yanga jana umekabidhi rasmi ofisi kwa uongozi mpya huku ukiacha deni la milioni 62 huku akaunti ikiwa na zaidi ya milioni 102.
Akizungumza leo katika hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika makao makuu ya klabu hiyo jana, aliyekuwa mwenyekiti wa Yanga Iman Madega aliutaka uongozi mpya kuendeleza mafanikio waliyoyafanya katika kipindi chao.
Akichanganua, Madega alisema wameacha zaidi ya milioni 102.Fedha hizo ni milioni 1,079,681.45 katika akaunti ya usajili, shilingi 795,629 katika akaunti ya mishahara, milioni 100, 978, 697 katika akaunti ya wanachama huku akaunti ya mwisho ya mishahara ya wachezaji na benchi la ufundi ikiwa haina kitu.
Aidha, kuna madeni yanayofikia kiasi cha shilingi mil 27, 977, 628 ambapo kiasi hicho kinajumuisha deni la sh 6,650,000 katika hoteli ya Tamal, deni jingine ni Mil.10,750,000 kwa kampuni ya All Sports Promotion; Mil.5.5 kwenye hoteli ya Valley View Hoteli, sh 500,000 kwa mdau aliyewauzia basi na sh 6,077,628.78 kwa Dawasco.
Aidha, Madega alitaja deni jingine waliloliacha kuwa ni dola 35, 000 zinazodaiwa na CECAFA na kusema kuwa ingawa deni hilo lilisimamishwa baada ya kukata rufaa CAS, viongozi wapya hawana budi kulifuatilia.
Mbali na hilo, Madega alimkabidhi mwenyekiti mpya Lloyd Nchunga Katiba mpya ya Yanga, Logo, mkataba wa miaka mitano wa TBL, mkataba wa mwaka mmoja wa matibabu toka kituo cha AMI, uwanja wa kaunda.
Pia majengo mawili ambalo moja lipo mtaa wa Mafia na jingine lililopo Jangwani na Twiga huku akisema lioxcha ya kufanya jitihada za kutafuta kadi zake lakini ilishindikana hivyo kuwaomba viongozi hao kuendelea kufuatilia.
“Pia tumeacha magari matatu, mawili ni yale yaliyotolewa na TBL na moja lililiharibika lipo katika yadi ya mmoja ya wanachama wetu Seif Mohammed”, Alisema Madega.
Naye Nchunga alishukuru kwa kitendo hicho cha kiungwana na kusema kuwa wataendeleza mazuri yaliyopo na pia kuomba ushauri pindi wanapohitaji.
Pamoja na kwamba siipendi yanga lkn sijaona uongozi uliowahi kuwacha pesa ktk akaunti wakati unatoka madarakani huu ndio wa kwanza kipato cha yanga hakina tofauti na cha simba na mechi wana cheza sawa tena yanga ilikuwa na wachezaji wengi wa kulipwa kuliko simba ebu angalia akaunti za simba zilivyoachwa na waliondoka hata milioni 1 hakuna ni madeni tu kibao. hongera sana madega na kikosi chako
ReplyDelete