Ramadhani karimu, leo imetuwasilia
Mwezi huu maalumu, usitende maasia
Funga swala zidumu, suna za kuendelea Waja tumefaradhiwa, kufunga ni sharuti
Mgonjwa aruhusiwa, msafiri yumo kati
Ndio walokubaliwa, kuzilipa kwa wakati
Ramadhani sana swali, kaburini upate huja
Saumu yahuisha mwili, daktari huna haja
Waua ndege wawili, kwa jiwe lako moja
Katika miezi sita, nafusio sidhulumu
Ramadhani hufuata, mengine huifahamu
Madhambi Rajabu wata, ukamilishe Muharamu
Tuikeshee tahajudi, tusome sana Qur’ani
Tuwe wenye kurudi, kutafuta sam ahani
Tukidhiwe nyuradi, kutiwa kesho peponi
Usishiriki shatani, kenda kuteza karata
Domo kaya masikani, ulimi wako fumbata
Kijipinda ibadani, utumalo utapata
Zikithirishe sadaka, mwezi huu mtukufu
Tajiri uitoe zaka, utakase mali uchafu
Utalipwa bila shaka, malipoe maradufu
Mato yako yadhibiti, usitizame haramu
Hasira zako zatiti, ukiwa kwenye saumu
Itikafu uiketi, msikitini udumu
Futirisha masikini, ukitarajia pepo
Japo hali taabani, jikune ujipatapo
Haipotei yakini, konde tende utowapo
Ewe mfanyi biashara, itunge sana mezani
Wateja kutopora, umuogope manani
Vya wendo kunyofora, akhera hiyo ni deni
Kesha kumi la mwisho, utafute usiku bora
Jaza yake hakikisho, miezi alfu moja mara
Malipo ya lako jasho, ya mwezi mzima subira
Mwezi utapo kwisha, kuifunga Ramadhani
Swala bado hazijesha, si mwisho wa Qur-an
Tujikaze kudumisha, ibada zetu duniani
Nawaombea wendani, Ramadhani makbuli
Msamaha kwa manani, twatumai takubali
Tumalize kwa makini, kufunga mwezi kamili
ASANTE JAMES BIBOZE
Hii safi sana jee nichukuwe nikaweke kwenye blog yangu
ReplyDeletebig up kwa kutuwekea ukaribisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, kumbe mara nyingine unakumbuka dini. mungu akubariki
ReplyDeleteEbou waweza copy mwenyewe nlitumiwa na mdau wangu james, Ramadhan Kareem
ReplyDelete