STARS
HARAMBEE STARS
Mechi hiyo ya kirafiki ya kimataifa iliyopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru ambapo Ngassa alisawazisha bao hilo katika dakika ya 57 baada kuuwahi mpira uliokuwa ukirejeshwa langoni na mchezaji wa Harambee, Julius Owino.
Shukrani ziende kwa kipa wa Stars, Shaban Kado ambaye aliweza kupangua mipira iliyoelekezwa langoni mwake ikiwemo shuti la mita 30 lililopigwa na Dennis Oliechi katika ya 60
Winga wa kulia wa Harambee anayekipiga katika klabu ya Inter Milan Macdonald Maliga anayekipiga katika klabu ya Inter Milan ya Italia ndiye aliyeifungia bao timu yake katika dakika ya 13 ya mchezo huo.
Maliga alipiga mpira wa adhabu baada ya Harambee bao la kwanza kwa mpira wa adhabu baada ya beki wa Stars, Kelvin Yondan kumchezea vibaya Dennis Oliechi.
Dakika ya 38 mshambuliaji wa Stars Mussa Mgosi alipiga shuti kali lililotoka juu ya lango baaada ya kupojkea pasi ya Uhuru.
Dakika tatu baadaye Oliech alipiga shuti la umbali wa mita 30 lakini Kado aliutoa nje.
Katika dakika ya 45 Mariga alipiga adhabu nyingine baada ya Yondan kumchezea Rafu John barasa lakini kipa kado aliupangua mpira ukatoka nje.
Katika kipindi cha pili Stars iliwatoa Uhuru Seleman, Yondan, Jabir Aziz, Abdi Kassim na Idrissa Rajab na kuwaingiza Agrey Morris, Seleman Kassim Abdulhalim Homoud , Athuman Iddi ‘Chuji’na Stefano Mwasika.
Mabadiliko hayo yaliipa uhai Stars, ambayo ilianza kulishambulia lango la Harambee, tofauti na awali walipokuwa wakiingia mara chache kutokana na mabeiki wa Harambee kuwa makini.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kocha wa Stars, Jan Paulsen ambaye ilikuywa ni mechi yake ya kwanza tangu aingie mkataba wa kuinoa alisema kipindi cha kwanza timu yake ilicheza vibaya lakini mabadiliko aliyoyafanya katyika kipindi cha pili yalisaidia kuleta uhai.
Naye kocha wa Harambee Tahir Muhidin alisema mechi hiyo imempa mwelekeo wa maandalizi ya mechi yake ya kuwania kucheza fainali za Afrika dhidi ya Guinea Bissau itakayopigwa Septemba 4.
Aliongeza kuwa Tanzania inakibarua kigumu katika kundi lake kutokana na kupwanga bna timu zenye wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya.
Stars:Kado, Idrissa / Mwasika, Shadrack Nsajigwa, Yondan/Seleman Kassim, Nadir Haroub ‘Canavaro’, Nurdin Bakari, Abdi /Chuji, Mrisho Ngassa, Jabir , / Humoud, Tegete/ Mgossi na Uhuru/Agrey Morris
Harambee:Wilson Obungu, Julius Owino, George Owino, Lloyd Wahome, Edger Ochieng, Patrick Ooko, Mc Donald Mariga, George Odhiambo/Allan Wanga, Deniss Oliech, John Barasa/ Anthony Kimani na Kelvio Omondi