MUSTAFA HASSANALI
Akizungumza mapema leo Mustafa alisema maonyesho hayo yatafanyika Septemba 16 na 17 katika ukumbi wa Diamond jubilee ambapo pia kutafanyika warsha ya kubadilishana ujuzi miongoni mwa washiriki.
Alisema lengo la maonyesho hayo ni kuendeleza na kuthamini mchango wa wanawake katika maendeleo ya Taifa kwa kutambua uwezo na mafanikio ya wanawake wajasiriamali, pamoja na wale wenye ulemavu ili kuleta ajira.
Aliongeza kuwa warsha hiyo pia inalenga kuonyesha wanawake wajasiriamali kama mfano wa kuigwa, kuongeza juhudi zao, kutoa ujumbe na kubadilishana mbinu nzuri za kibiashara.
“Pia kuwajenga wafanyabiashara wanawake kwa kuanzisha TWENDE SACCOS, kuendeleza uzalendo wa kutumia bidhaa za Tanzania, kutengeneza jukwaa kwa ajili ya wanawake wenye uwezo mdogo, wa kati, mkubwa na wale wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) kuweza kuonyesha bidhaa na huduma na huduma zao kwa pamoja kwenye mpangilio mzuri”, Alisema.