SAM Timbe kutoka Uganda ndiye amerithi mikoba ya Mserbia Kostadin Papic kuinoa klabu ya Yanga.
Timbe kocha aliyewahi kuzinoa timu mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki na Bara Asia ametambulishwa rasmi kwa wanahabari asubuhi ya leo katika ofisi za mfadhili wa timu hiyo, Yussuf Manji.
Akizungumza katika mkutano huo, Timbe alisema amekuja kuisaidia Yanga kupata mafanikio lakini kikubwa ni ushirikiano baina ya wachezaji, viongozi na wanachama kwa ujumla.
Hata hivyo kocha huyo bado hajasaini mkataba na Yanga inagawa mazungumzo yapo katika hatua nzuri.
إرسال تعليق