SHIRIKA la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limekipiga tafu ya sh milioni 3 Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ili kukifanikishia kushiriki kongamano la waandishi wa habari duniani litakalofanyika Machi 22 hadi 27 Korea Kusini.
Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jijini Dar es Salaam kati ya Ofisa Habari Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu, na Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Maulid Kitenge, ambaye ndiye atakayekiwakilisha chama hicho katika kongamano hilo.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Kintu alisema fedha hizo zitagharamia tiketi kwa ajili hiyo, hasa baada ya kutambua mchango wa waandishi wa habari katika nyanja ya maendeleo.
Kintu alisema Kitenge ni mmoja wa wadau wanaoitangaza NSSF katika nyanja ya maendeleo hapa nchini.
Naye Kitenge kwa upande wake, aliishukuru NSSF kwa msaada huo ambao utamwezesha kwenda na kurejea katika kongamano hilo ambapo anatarajia kuondoka nchini Machi 21 huku akiahidi amedhamiria kuwaunganisha waandishi wa habari wa Tanzania na wengine.
Kitenge alisema Kamati ya Utendaji ya TASWA, pia itampa mapendekezo ambayo atayawasilisha katika mkutano huo.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando ‘Mgosi’, aliishukuru NSSF kwa msaada huo, ingawa waliomba katika kipindi cha muda mfupi.
Mhando alisema, katika kongamano hilo Kitenge ataambatana na Katibu Msaidizi, George John, na kutoa wito kwa wadau kumsaidia naye afanikishe safari yake hiyo.