MFALME wa nyimbo za asili nchini, Costa Siboka, kesho anatarajiwa kupamba fainali za mashindano ya Ngoma za Asili mkoani Mwanza, yatakayofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.
Akizungumza kwa simu kutoka Mwanza, Siboka alisema kupitia onyesho hilo mashabiki watapata burudani ya aina yake kutoka kwake sambamba na kundi lake.
Alisema pamoja na burudani hiyo pia mashabiki wake watapata nafasi ya kupata burudani ya kazi zake mpya pamoja na kuwashuhudia wanenguaji wake wapya wakiwamo Halima Ndembendembe, Fadhira Mitikisiko, Salama Kadogoo na Queen Mwanasesere, ambao wamepata mafunzo kutoka Chuo cha Sanaa Bagamoyo.
“Mashabiki wangu wa huku nashukuru kwa kunipokea kwa wingi, pia kuzikubali kazi zangu, mambo yote kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba,” alisema.