BOB HAISA KUSAMBAZA MWENYEWE ALBAMU YAKE


MWANAMUZIKI maarufu wa miondoko ya mduara, Haisa Mbyula, ‘Bob Haisa’ amesema atasambaza mwenyewe albamu yake mpya inayofahamika kwa jila la ‘Meza ya wanandoa’ kwa ajili ya kukwepa bei kubwa ya wasambazaji wakubwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mbyula alisema kuwa anasambaza albamu hiyo kwa bei ya chini ili kila mmoja aweze kuinunua kwasababu wasambazaji wamekuwa wakiuza kwa bei kubwa hali inayofanya kutouzika.
Mbyula alisema kuwa kutokana na usambazaji anaoufanya albamu hiyo imekuwa inauzika kutokana na kuuza bei halali inayotakiwa kuuzwa na wasambazaji wakuu ambao kuuza kwao kwa bei ya juu kumefanya watu washindwe kununua kazi zake.
Alisema baada ya kumaliza taratibu za usambazaji anatarajia kufanya tamasha la wanandoa kwenye mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuwakutanisha wanandoa, waliotoka kwenye ndoa na wale wanaotaka kuingia kwenye ndoa.
Mbyula alitaja nyimbo zilizopo katika albamu hiyo kuwa ni pamoja na Chereko leo, Mama wa Biharusi, Olile Oshasha, Maisha ya Ndoa Bhatoja, Tukate keki, Sombelagi na hongera wazazi.

Post a Comment

Previous Post Next Post