TWIGA STARS KUJARIBU NAFASI YA TATU KESHO


TIMU ya soka ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’, kesho inashuka katika dimba la Rufaro, Zimbabwe, kukwaana na Malawi katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu ya michuano ya COSAFA.
Twiga inawania nafasi hiyo baada ya jana kufungwa kwa penalti 4-2 na wenyeji Zimbabwe katika mechi ya nusu fainali, ambapo dakika 90 timu hizo zilimaliza kwa suluhu ya bila kufungana, huku Malawi ikitinga hatua hiyo baada ya kufungwa mabao 5-1 na Afrika Kusini.
Katika mechi ya juzi, mshambuliaji mahiri, Asha Rashid ‘Mwalala’ alikosa penalti katika dakika ya 44 iliyookolewa na kipa Onai Chingawo, ambapo mwamuzi Gladys Lwengwe wa Zimbabwe alitoa adhabu hiyo baada ya Mwanahamis Omari kuangushwa katika eneo la hatari na beki wa Zimbabwe, Eunice Chibanda, ambaye pia alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Sophia Mwasikili na Mwanahamis Omari walipata penalti zao huku Fatuma Khatib na Fatma Makusanya wakikosa.
Kocha Mkuu wa Twiga, Charles Boniface Mkwasa, amekifanyia marekebisho madogo kikosi chake ili kuhakikisha kinashinda mechi yake ya leo.

Post a Comment

Previous Post Next Post