SIMBA, YANGA FAINALI KOMBE LA KAGAME



FAINALI ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati ‘Kagame Castle Cup 2011’   itawakutanisha watani wa jadi katika soka ya Tanzania, Simba na Yanga  keshokutwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Hiyo inafuatia ushindi wa penalti 5-4 iliyoupata Yanga leo dhidi  ya St. George ya Ethiopia, baada ya kutoka sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 katika mchezo wa  nusu fainali ya pili ya michuano hiyo.
Ikumbukwe jana Simba iliitoa timu ngumu katika ukanda huo, El Mereikh ya Sudan kwa changamoto ya penalti 5-4, baada ya kutoka sare 1-1 ndani ya dakika 120.
Mchezo wa jana ulianza kwa kasi  ambapo sekunde ya 52 nusura Isaack Isinde wa St. George atikise nyavu za Yanga baada kubaki na kipa lakini alipiga shuti hafifu, lililookolewa na kipa wa Yanga, Berko, Yanga ilijibu shambulizi hilo katika dakika ya 10 kupitia kwa Jerry Tegete lakini mpira ulikuwa mwingi na ukatoka.
Timu hizo ziliendelea na mashambuliana kwa kupokezana huku wachezaji wake wakishindwa kuzitikisa nyavu katika vipindi tofauti, licha ya kupata nafasi bwererere za kufanya hivyo na kushindwa kuzitumia vizuri.
St. George ilipata nafasi nyingine dakika ya 16, 18 na 20 kupitia kwa Suleiman Mohammed na Salhadin Said, lakini walipiga pasi fyongo, huku Yanga nayo kupitia kwa Davies Mwape na Chacha Marwa ikishindwa kutumia nafasi ilizozipata katika dakika ya 28 na 33, kwani  mabeki wa St George waliokoa hatari hizo.
Mechi hiyo iliyokuwa kitendawili cha nani atatinga nusu fainali ya michuano hiyo ilimaliza kwa dakika 90 kwa sare ya bila ya kufungana hivyo mwamuzi kuongeza dakika 30 nyingine zilizomalizika kwa matokeo hayo hayo na ndipo ilipokuja changamoto ya penalti.
Beki wa Yanga Shadrack Nsajigwa alianza kwa kukosa penalti, huku Nadir Haroub, Juma Seif, Mwape, Hamis Kiiza na Nurdin Bakari wakipata, wakati Abebaw Butako, Degu Debebe, Isaac Isinde, Alula Girma walipata kwa upande wa St. George, huku Salahadin Said na Anthony Bongole wakikosa.
Simba na Yanga watakutana kwa mara ya pili katika fainali ya michuano hiyo tangu kuanza kwake ambapo  mara ya mwisho ilikuwa mwaka 1992 Visiwani Zanzibar na Simba kushinda kwa penalty, baada ya kutoka sare ya 1-1 ndani ya dakika 120.
Wakati mahasimu hao wakikutana katika fainali, El Hillary na St. George watakwaana katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Rais wa Kagame na mdau mmoja kutoka nchini Sudan.
Yanga: Yaw Berko, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Oscar Joshua, Chacha Marwa, Nadir Haroub ‘Canavaro’, Nurdin Bakari, Jerry Tegete/Rashid Gumbo, Davies Mwape, Juma Seif na Kigi Makasi/HAmis Kiiza.
St. George: Robert Odonkara, Degu Debebe, Abebaw Butako, Alula Girma, Isaac Isinde, Yared Zinabu, Michael Desta, Abdulkarim Hassan, Salahadin Said, Prince Godwin na Suleiman Mohammed/Sula Matovu.

4 Comments

  1. NILIJUWA KICHWA CHA HABARI UTAKACHO ANDIKA LEO KITAKUWA CHA KAWAIDA...ILA INGEKUWA SIMBA UNGEANDIKA WERAWERA...DUU..NAONA UMEANDIKA KWA UNYONGE USIJARI ....YANGAA OYEEEEE... CCM OYEEE..BADO JUMAPILI TENA TUTAKAVYO MSALAMBATISHA MNYAMA KWA KISHINDO......
    MDAU HAPA FROM USA

    ReplyDelete
  2. utajibeba kama tunaipenda Simba inahuuuu, hahaha utasema sana habari ndiyo hiyo na wala hulazimishwi kusoma habari zetu

    ReplyDelete
  3. Oh yes, sina muda mchafu...kwanza sura zenu siyo nzuri...lol

    ReplyDelete
  4. hahaha na utakereka sana huna lolote wewe utakufa na kijiba kwa sura gani uliyonayo mjinga wewe kama mzuri zaidi yetu jitokeze, nadhani wewe ni 'wifi' ndiyo maana unatuonea donge, lol

    ReplyDelete
Previous Post Next Post