SIMBA SC YAPATA MSEMAJI MPYA


Adobe Systems SIMBA SPORTS CLUB            
P.O.BOX 15318 | TEL+255 2120754 | FAX+255 22 2120755|MSIMBAZI/MCHIKICHI STREET | DAR ES SALAAM | TANZANIA | AFFILIATED TO TFF, DRFA and IDFA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


KLABU ya Soka ya Simba leo inatangaza uteuzi wa Ezekiel Kamwaga (31) kuwa Ofisa Habari wa klabu.

Kabla ya uteuzi huo, Kamwaga, alikuwa Mhariri wa Habari wa gazeti la kila wiki la MwanaHALISI na ana uzoefu wa fani ya uandishi wa habari na mahusiano ya umma wa takribani miaka kumi; akifanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya nchi.

Ninaamini kuwa kwa uteuzi huu ambao uanziba nafasi iliyokuwa wazi kwa takribani miezi miwili, klabu yetu imeonyesha imani kubwa iliyonayo kwa vijana ambao wakichanganya maarifa yao na busara, hekima na mwono wa wazee wetu, Simba itazidi kuwa klabu ya kisasa, inayoendeshwa kisayansi na mfano wa kuigwa si tu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati, bali Afrika kwa ujumla.

Ninawaomba wapenzi na wanachama wa Simba, vyombo vya habari na wadau wote wa michezo nchini watoe ushirikiano wa kutosha kwa mfanyakazi wetu mpya ili dhumuni la kuboresha soka letu na sekta ya michezo kwa ujumla nchini litimie.

Imesainiwa
 Evodius Mtawala
 Katibu Mkuu
 08 Julai 2011

Post a Comment

Previous Post Next Post