
UWANJA wa kisasa unaotarajiwa kujengwa na klabu ya soka ya Simba ‘Simba Sports Arena’ unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi bil.75 za kitanzania, utakuwa na sehemu za kufanyia manunuzi, hoteli, kumbi mbili za mikutano kwa ajili ya watu mashuhuri ‘VIP’ ambapo kila ukumbi utakuwa na uwezo wa kuingiza watu 80, pamoja na mgahawa utakaoingiza watu 250.