KASEJA:WYDAD CASABLANCA WAMETUFUNGA KWA UZEMBE WETU

KIPA namba moja wa timu ya soka ya Simba Juma Kaseja (Pichani kushoto) amesema kufungwa kwao kulitokana na kupoteza umakini kwa wachezaji wa timu hiyo ndipo kulipelekea kufungwa mabao 3-0 na Wydad Casablanca, jumamosi mjini Cairo,Misri.
Akizungumza mara baada ya kuwasili kutoka Misri, Kaseja alisema mechi hiyo ilikuwa 50/50 lakini kwa bahati mbaya walifungwa  kutokana na kupoteza umakini katika dakika hizo za mwisho, katika mechi yao hiyo iliyokuwa ya kuwania kucheza nane bora ya ligi ya mabingwa Afrika.
"Ni makosa ya kawaida tu na hapaswi kulaumiwa mtu yoyote, huuu sio muda wa kuweza kumlaumu mtu bali timu nzima imefanya makosa na hivyo kupoteza,tuachanane na matokeo hayo na kujipanga na mechi inayofuata".
Akiizungumzia  Wydad alisema ni timu ya kawaida ingawa imewazidi kwa kiasi kifulani
Simba itakutana na Motema Pembe katika mechi ya kuwania kombe la Shirikisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post