TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Juni 15, 2011
TFF, VILLA SQUAD KUKUTANA KESHO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kesho (Juni 16 mwaka huu) atakutana na wadau mbalimbali ili kuangalia mustakabali wa klabu ya Villa Squad ambayo msimu huu itashiriki Ligi Kuu ya Vodacom.
Mkutano huo utafanyika makao makuu ya TFF kuanzia saa 9 kamili.
Mbali ya Rais Tenga na Sekretarieti yake, wadau wengine katika mkutano huo ni wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kamati ya Uchaguzi ya Villa Squad na viongozi wa klabu hiyo.
Boniface Wambura
Ofisa Habari