ALIYEKUWA kiungo wa timu ya soka ya Simba Mohammed Banka amesema hatochezea timu yoyote katika msimu mpya wa ligi kuu bara badala yake anaelekeza akili yake katika timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.
“Siendi kuichezea timu yoyote kwa sasa na wala sina mpango wa kucheza katika katika msimu ujao wa ligi sana nitaelekeza nguvu zangu katika timu ya Taifa tu,”Alisema Banka.
Banka amefikia hatua hiyo baada ya uongozi kumhamishia kwa mkopo katika klabu ya soka Villa Squad ya jijini Dar es Salam na kusema kuwa maamuzi hayo yanatokana na viongozi wake kutomshirikisha katika maamuzi hayo kitendo ambacho si cha kiungwana.
“Si kama naidharau Villa au la ni kwamba kitendo cha kupelekwa katika timu bila makubaliano yoyote ndicho kimenisikisha mimi, kwanini viongozio wasizungumze na mimi kwanza kabla ya kuchukua uamuzi huu?Alihoji Banka.
Banka alisema, kutokana na hatua hiyo kwa sasa anaendelea kuangalia upande mwingine wa maisha yake zaidi ya soka ambapo atakuwa tayari kujiunga na timu atakayokubaliana nayo katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mbali na Banka, wachezaji wengine waliotolewa kwa mkopo kutoka Simba kwenda klabu zingine ni Aziz Gilla na Mbwana Bakari (Coastal Union), Mohamed Kijuso na Haruna Shamte (Villa Squad), Meshack Abel (Ruvu Shooting), Juma Jabu, Andrew Kazembe, Paulo
Terry na Godfrey Wambura (Moro United).
Aidha, Azam imewatoa Sino Augustino na Selemani Kassim ambao wanakwenda African Lyon na Tumba Louis (Moro United), wakati Yanga imewapeleka wachezaji wake Omega Seme na Idd Mbaga kwa mkopo African Lyon.
Kama achezi kwenye timu yoyote, Taifa stars aisahau, Poulsen aiti mchezaji asiye na timuKama achezi kwenye timu yoyote, Taifa stars aisahau, Poulsen aiti mchezaji asiye na timu
ReplyDelete