'THERE IS ONLY ONE KASEJA', AIPELEKA SIMBA FAINALI KOMBE LA KAGAME

 ILIKUWA  ni hoihoi nderemo na kila aina ya vifijo leo kwenye uwanja wa Taifa,  Dare s Salaam kwa mashabiki wa Simba SC baada ya mlinda mlango wake  Juma Kaseja (Pichani)kupangua mkwaju wa penalti wa mshambuliaji wa El Mereikh ya Sudan Jonas Sakwaha na kuifanya Simba itinge fainali ya klabu bingwa ya Afrika Mashariki na Kati ‘Kagame Castle Cup’  kwa ushindi wa penati 5-4 baada ya sare ya bao 1- ndani ya dakika 120. 
Kana kwamba alijua anakwenda kuipangua penalti hiyo, shujaa wa kucheza michomo hiyo Kaseja aliwaelekea mashabiki wa Simba na kuwaonyesha ishara ya kuwataka wainuke washangilie wakati Sakwaha anakwenda kupiga naye anakwenda kusiamma langoni.
 Na kweli, kwa kujiamini na kwa umahiri mkubwa Kaseja aliyejiunga na Simba mwaka 2003 aliicheza penalti hiyo na kuufanya uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kukuisanya mashabiki 60,000 ulipuke kwa shangwe.

Baada ya hapo Kaseja alivua jezi yake na kubaki na fulana nyeupe yenyemaandishi yaliyokuwa ‘There is Only One Kaseja’ yakimaanisha, kuna Kaseja mmoja ukiwa ni ujumbe kwa mashabiki na wadau ambao wamekuwa wakibeza kiwango chake licha ya umahiri wake wenye kusadikika.


Katika mechi hiyo Adiko Rime ndiye alianza kuifungia El Mereikh bao la kuongoza katika dakika ya 12 akiunganisha pasi ya Jonas Sakwaha, kabla ya Ulimboka Mwakingwe kuisawazisghia Simba katika dakika ya 24 kwa kichwa baada ya kipa wa El Mereikh kumponyoka mpira wa krosi ulipigwa na Shija Mkina

Dakika 90 zilimalizika kwa sare ya bao 1-1 hivyo mwamuzi kuonmgeza dakika 30, ambazo nazo zilimalizika kwa matokeo hao na hivyo kuamuliwa  changamoto ya mikwaju ya Penati

Katika hatua ya Penalti, waliopata kwa ipande wa Simba ni Jerry Santo, Salum Kanoni, Nassoro Said, Patrick mafisango  na Mwakingwe, huku Salum Machaku akikosa.
Faisal Sido, Ahmed Albasha, Badr Eldod, Isam Elhadary walipata kwa upande wa El Mereikh huku waliopata ni Sakwaha na Collins Kelechi.

Mara ya mwisho Simba kuingia fainali ya michuano hiyo ilikuwa mwaka 2003 ilipofungwa 1-0 na Sc Villa Kampala, mwaka huo walikuwa mabingwa watetezi wakitoka kuchukua ubingwa Visiwani Zanzibar kwa kuifunga Prince Luis ya Burundi bao 1-0 lililofungwa na Nteze John Lungu.
Simba:Juma Kaseja, Nasoro Said, Amir Maftah/Salum Kanoni, Juma Nyoso, Kelvin Yondan, Patrick Mafisango, Jerry Santo, Shija Mkina, Haruna Moshi/Rajab Isihaka, Ulimboka Mwakingwe na Musa Mgosi/Salum Machaku.
 El Mereikh:Osam Elhadary, Saeed Mustafa, Nagm Eldin Abdallah, Adiko Rime/Collins Kelechi, Ahmed Elbasha, Badr Eldin, Mohamed Mugadam/Faisal Agab Sido, Jonas Sakwaha, Musab Omer/Worgu Stephen, Nasr Eldin Omer na Balla Gabir.

2 Comments

  1. Kesho naomba uandike na habari za YANGA KWA MBWEMBWE USIPOFANYA HIVYO NITAJUWA WE KWELI NI MNAZI WA SIMBA DAMU!! BALAAA...ngoja jumapili atajuwa kuwa KUNA CHAMA CHA SIASA KIMOJA TU NI CCM NA TIMU MOJA TU NI DAR YANGA AFRICAN..... YANGA KESHO TUNAFUNGA MTU 2bila ..wakafe na njaa huko kwao ethiopia......

    ReplyDelete
  2. Wewe humjui huyu dada kama ni Simba? mimi huwa nikiona habari za michezo zilizoandikwa na huyu dada, au Somoe, Mayembe na mwingine anaitwa Mwani huwa naacha hata kusoma, yaani wanaboa hawa wenyewe hata Simba kafanya vibaya wanasifu tu, ni chuo gani mlisomea uhandishi wa habari??

    Mdau
    Finland

    ReplyDelete
Previous Post Next Post