WAREMBO wanaotarajiwa kuwania shindano la kumsaka Redd’s Miss Kinondoni wanatarajiwa kuingia kambini keshi katika hoteli ya Giraffe Ocean View.
Mkurugenzi wa Boy George Promotions inayoandaa shindano hilo, Rahma George amewataja warembo hao kuwa ni pamoja na Fatma Pongwa, Winnie Gerald, Mariam Almas, Stellah Premsing, Hamisa Hassan, StellaMbuge, HUsna MAulid, Felister Philip, Stella Morris, Naomi Jones, Pamela Gordian, Renalda Apojei na Sabrina Abdallah.
Rahma alisema warembo hao watakuwa wakinolewa na Miss Tanzania mwaka 2007, Richa Adhia ambapo shindano limepangwa kufanyika Julai 23 katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Kazi kwao washindwe wenyewe! Tupo pamoja kama kawa!
ReplyDelete