ANGALIZO KWA WATANZANIA WOTE, UTAPELI HUU UNAANZA KUOTA MIZIZI

KUNA TAARIFA ZA WANIGERIA AMBAO WAMEWEKA MASKANI MAENEO YA SINZA, SHUGHULI AMBAZO WANAFANYA WANAIGERIA HAWA BADO HAZIELEWEKI, NI TATA.

MUDA MWINGI HASA VIPINDI VYA JIONI WANAPENDA KUSHINDA KATIKA BAA KADHAA AMBAZO ZINA AMBAA AMBAA NA BARA BARA YA SHEKILANGO, KUANZIA MAENEO YA URAFIKI MPAKA BAMAGA.
HIVI KARIBUNI WATUMIAJI WENGI WA SIMU ZA KIGANJANI NA INTERNET WAMEKUWA WAKITUMIWA MESEJI MBALI MBALI ZA KUSHINDA ZAWADI FLANI, MFANO WATUMIAJI WA SIMU ZA KIGANJANI WAMEKUWA WAKIPATA MSG AMBAYO INAWAONYESHA WAMESHINDA ZAWADI KUTOKA KAMPUNI YA NOKIA, WAKATI UNAKUTA ULIOTUMIWA MSG HIYO MUDA HUO UNATUMIA SIMU YA MCHINA AMBAYO HAINA HATA JINA, NA WALE WATUMIAJI WA INTERNET WANAPATA EMAIL ZA KUTAKA WAINGIZE DETAIL ZAO ZA AKAUNTI ZAO ZA BENKI, HIYO EMAIL INAKUONYESHA KAMA VILE ULICHEZA BAHATI NASIBU FLANI.
WATANZANIA WOTE KAENI CHONJO, KAPINGAZ Blog BADO INAWAFUATILIA HAWA JAMAA ILI KUWEZA KUJUA UNDANI WAO, NA VILE VILE TUNAVIOMBA VYOMBO VYA USALAMA NAVYO VIWEZE KUJUA HAWA JAMAA WANAFANYA NINI, HOFU YETU INAWEZEKANA WAO NDIO WANAJIHUSISHA NA UTAPELI HUU AMBAO NAAMINI WATANZANIA WENGI BADO HAWAJAUJUA VIZURI WIZI HUU WA KUTUMIA MITANDAO.

Post a Comment

Previous Post Next Post