SHAMBA LA BIBI KUBEBA SHEREHE ZA MIAKA 50 YA UHURU

Matengenezo ya Uwanja wa Uhuru  yanatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu ambapo  maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na shughuli nyingine zitaendfelea kufanyika katika uwanja huo.
Msimamizi wa ujenzi wa uwanja huo kutoka serikalini, Aloyce Mushi, kutokana na kasi iliyoongezwa, ujenzi huo unatarajiwa kumalizika katikati ya mwezi ujao, hivyo wana uhakika kuwa maadhimisho hayo yatafanyika uwanjani hapo.
"Hakuna wasiwasi maadhimisho hayo yatakakofanyika kutokana na kutokamilika kwa uwanja huo, ambako alisisitiza na kuwahakikishia Watanzania kuwa, maadhimisho hayo yatafanyika kwenye Uwanja huo kutokana na hatua waliyofikia,"Alisema.

Post a Comment

Previous Post Next Post