YANGA WAIPUMULIA NYUMA SIMBA

BAO pekee la mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Kiiza Hamisi 'Diego' leo limeipa ushindi wa 1-0 Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha kwenye Uwanja wa Azam, Chamazi, Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe pointi 21 baada ya kucheza mechi 11 na kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo, ikiwa inalingana kwa pointi na Azam FC, lakini yenyewe inakuwa juu kwa wastani wake mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Yanga itakuwa nafasi ya kuwakaribia vinara wa ligi hiyo, Simba SC Jumamosi wakati watani hao wa jadi katika soka ya Tanzania watakapomenyana, Uwanja wa Taifa. Simba ina pointi 27 baada ya kucheza mechi 11 pia.

Post a Comment

Previous Post Next Post