KIUNGO mshambuliaji wa Simba anakusudia kuvishtaki vymbo vya habari vilivyoeneza taarifa kuwa alimpiga mchezaji mwenzake, Emmanuel Okwi,mara baada ya kumalizika kwa mechi ya ligi kuu baina yao na Yanga ambapo Simba iliaambulia kichapo cha bao 1-0.
Baban amesema anashangazwa na taarifa hizo za uzushi zenye lengo la kumpaka matope hivyo atawachukulia sheria wote wal;iohusika ili kutoa fundisho kwa vyombo vingine vya habari ama watu wanaopenda kupaka matope watu bila sababu za msingi.
Ilidaiwa kuwa, Boban alifikia hatua ya kumchapa makofi Okwi kwa madai kuwa amekuwa akiikosha magoli timu yakle pindi wanapokutana na mahasimu wao.